Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome,Int.34P, Via Gorgona 48, 00139 Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Wednesday, November 19, 2014

WATANZANIA ITALY WAKUTANA NA MAKAMU WA RAIS MHESHIMIWA MOHAMED GHARIB BILAL MJINI ROMA

 Siku ya jana, tarehe 18 Novemba 2014 kwa Watanzania Italy, imeingia kwenye historia baada ya Watanzania Italy kupata fursa ya kukutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Mohamed Gharib Bilal . Mkutano  ulidhuliwa na msafara mzito aliokuja nao Makamu wa Rais, balozi wa Tanzania nchini Italy Mh. James Alex Msekela, maofisa wa ubalozi, viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Tanzania nchini Italy pamoja na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italy. 
 
 
 
Gari lililombeba Makamu wa Rais, Mheshimiwa Mohamed Gharib Bilal. Hapa likiwa limepakiwa katika Hotel ya EDEN. Hotel aliyofikia Mh. Makamu wa Rais.

Mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora Italy, Mh. Maulid Kagutta akitoa risala kwa niaba ya Wanadiaspora Italia.

Meza Kuu Wakati wa Mkutano kama inavyoonekana.

Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. James Alex Msekela akipata picha pamoja na Makamu wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mama Bilal.

Watanzania wakisalimiana na Makamu wa Rais.

Picha ya pamoja na Makamu wa Rais.


Kwa yeyote ambaye anapicha zaidi za tukio ili tafadhali anitumie  kwenye e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it ili tuweze kuzitundika!
 

Sunday, November 16, 2014

ZOEZI LA MAOMBI YA PASIPOTI LINAENDELEA MJINI NAPOLI

Maofisa wa Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam na Zanzibar wameanza zoezi la kupokea maombi ya pasipoti kutoka kwa Watanzania waliopo Italy. Maofisa hao wanategemewa kuelekea Turkey na Greece,kwa ajili hiyo hiyo. Haya ni matunda ya Kamati ya Diaspora ilyokutana na Mh Balozi James Alex Msekela, mwezi juni mwaka huu. Kamati ilikutana na balozi na maofisa wa juu wa kibalozi kwa ajili ya kutambulisha kamati na uongozi wake,na pia kuwakilisha kero na matatizo ya watanzania wanaoishi Italy kwa jumla. Mkutano huo uliisha kwa mafanikio makubwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya uchapa kazi wa kweli wa mh Balozi, kwani katika mapumziko yake nchini Tanzania mwezi August alitumia muda wake kukutana na Kamishna wa Uhamiaji Tanzania kujadili suala la matatizo ya Pasipoti kwa watanzania wa Maeneo ya uwakilishi wake.

Source: JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA (JUWATAI) http://watanzaniaitalia.blogspot.it/2014/11/zoezi-la-maombi-ya-pasipoti-linaendelea.html?spref=fb
TANZANIA ITALIA SOCIETA' COOPERATIVA


MUDA NA SEHEMU YA KUKUTANA NA MAKAMU WA RAIS MH. MOHAMED GHARIB BILAL
TAREHE:  18/11/2014.
VENUE: HOTEL AMBASCIATORI PALACE
 MTAA: VIA VITTORIO VENETO 62, 00187 ROME

NB: WATAKAO FIKA, WANATAKIWA KUWA WAMESHAKAA UKUMBINI 
        IFIKAPO SAA TISA MCHANA TAYARI KWA MKUTANO.

Friday, November 14, 2014

Wednesday, November 12, 2014

Monday, November 10, 2014

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA MOHAMED GHARIB BILAL MJINI ROME 17-22 NOVEMBA 2014


 

Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, unapenda kuwatangazia Watanzania wote muishio nchini Italia kuwa, kutakuwa na ugeni mzito wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mohamed Gharib Bilal. Makamu wa Rais atawasili mjini Rome tarehe 17 Novemba na atakaa mpaka tarehe 22 Novemba kwaajiri ya kongamano la Kimataifa la Lishe katika ukumbi wa FAO. Mheshimiwa Makamu wa Rais anatarajiwa kukutana na Watanzania waishio Italia tarehe 18 Nov. 2014. Muda na sehemu ya mkutano, ubalozi utatufahamisha pale maandalizi yatakapo kuwa yamekamilika!

Sunday, June 22, 2014

HARUSI YA NDUGU YAKUBU KIPWATE NA AGNES WAMBUI YAFANA MJINI ROMA

JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA AMBAYO NDIO ILICHUKUA JUKUMU LA KUSIMAMIA HARUSI HII,  INAPENDA KUWASHUKURU WALE WOTE WALIOSHIRIKI KWENYE MAANDALIZI YA HARUSI.  PICHA ZAIDI ZITAFUATA KESHO! MUNGU WABARIKI MAHARUSI WETU, MUNGU IBARIKI JUMUIYA YETU!!                                


                                       

                                         

                                       
                                           


Friday, June 20, 2014

VIONGOZI WA "TANZANIA DIASPORA ITALIA" WAJITAMBULISHA KWA BALOZI


Balozi Dkt. James A. Msekela (aliyeketi katikati), pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wa Roma, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa ‘Tanzania Diaspora in Italy’ waliokuwa wamefika kujitambulisha. Aidha, siku hiyo ya tarehe 14/06/2014, viongozi hao walipata pia fursa ya kufanya kikao na Mhe. Balozi, ambapo kero na changamoto za watanzania nchini Italia zilizungumzwa. Kikao hicho kilikuwa cha mafanikio.

Sunday, May 11, 2014

BALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA MH. JAMES MSEKELA MKUTANONI INCHINI UTURUKI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe wa tatu kutoka kushoto na ujumbe wakijadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano na Uturuki na ujumbe wa Uturuki.

Waziri Membe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia anawakilisha Uturuki aliyekaa kushoto pamoja na Bw. Salvator Mbilinyi, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia aliyechuchuma, wakibadilishana machache katika chumba cha wageni maalum ndani ya Uwanja wa Ndege wa Ankara.